Mwakilishi wa wadi ya Magenche eneo bunge la Bomachoge katika kaunti ya Kisii Timothy Ogugu amewaomba wahandisi kuzitembelea barabara zote zinazoendelea kukarabatiwa katika kaunti hiyo ili kuthibitisha jinsi zinakarabatiwa.
Wito huo umetolewa baada ya kusemekana kuwa baadhi ya wanakandarasi hupewa kazi ya kukarabati barabara na kuzikarabati kwa njia isiyo halali na pia kukawia kumaliza ukarabati huo kinyume na muda wa maelewano.
Alikuwa akiyaongea haya siku ya Jumapili wakati alikuwa anatembelea barabara inayoendelea kukarabati katika wadi yake; kutoka Mokubo kuelekea Motaranda, na kusema kusema kuwa barabara hiyo haijmfurahisha jinsi inakarabatiwa.
Pia mwakilishi huyo aliomba wanakandarasi wote kuhakikisha wamekarabati barabara kwa muda wa maelewano, kando na kujiongezea wakati ili maendeleo kuafikiwa kwa wakati unaofaa
“Naomba wahandisi wa barabara katika kaunti yetu ya Kisii kuanza kutembelea barabara zinazoendelea kukarabatiwa kwa kaunti hii ili kuangalia jinsi barabara hizo zinakarabatiwa,” alisema Ogugu.
“Kwa upande wangu sioni kama barabara hizi zinakarabatiwa kwa njia ya halali, wakati mwanakandarasi anapewa kandarasi ya kutengeneza barabara, anastahili kuhakisha anakarabati vizuri kulingana na kiwango kile kinahitajika na kumaliza kwa muda wa maelewano,” aliongezea.