Wasimamizi wa shule ya Msingi ya Matutu, Wadi ya Gesima wamewaomba wahisani na wasamaria wema kuwasaidia kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea siku ya Ijumaa na Mwaandishi huyu, mwenyekiti wa shule hiyo George Onsare ilioko katika Wadi ya Gesima eneo Bunge la Kitutu Masaba, Kaunti ya Nyamira, aliwaomba wahisani kuwasaidia ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.

"Naomba wahisani kutusaidia kwa njia ya fedha au vifaa vya ujenzi tukamilishe ujenzi wa shule hii ili wanafunzi waweze kupata mahali pa kusomea," alihoji mwenyekiti Onsare.

Aidha, Onsare aliwapongeza wazazi kwa ushirikiano wao na kuwaomba waweze kuendelea vivyo hivyo hadi ujenzi huo ukamilike.

Kwa upande mwingine, alimwomba Mbunge wa Kitutu Masaba Timoty Bosire kuwasaidia na pesa za CDF ili ujenzi huo ukamilike haraka.

"Namuomba Mbunge wetu Bosire atusaidie tena pesa za CDF ili tuweze kukamilisha ujenzi wa madaraza ndio watoto wa eneo hili wapate mazingara mazuri wanaposoma," aliongezea Onsare.

Shule hiyo ilianza kujenga daraza mpya baada ya madarasa ambayo yamekuwa zaidi ya miaka 50 kuonyesha ishara ya kuporomoka.