Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wahudumu wa magari katika eneo la Kiambu wameonywa dhidi ya kuwaita abiria kwa sauti ya juu kwa kuwa ni kinyume na sheria.

Hii ni kufuatia kesi za hivi majuzi ambapo wahudumu hao wamekuwa wakitiwa mbaroni kwa hatia hilo.

Wahudumu hao kwa muda mrefu wamekuwa wakitoka kwa faini isiopungua elfu tano. 

Akizungumza katika ofisi yake siku ya Ijumaa, mkuu wa polisi katika kaunti ndogo ya Kiambu, Stephen Ng'etich alisema kwamba kesi za wahudumu hao wa magari zimekuwa zikishuhudiwa kila siku.

Ng'etich alieleza kwamba wahudumu hao hukiuka sheria hiyo hasaa wakati wa asubuhi na jioni. Alieleza kwamba wengi wa wale wanaotiwa mbaroni ni wale ambao wanapewa vibarua vya kujaza abiria kisha wanalipwa huku wengi wao wakikamatwa wakiwa walevi. 

Hata hivyo, mkuu wa polisi aliwahimiza wenyeviti wa shirika za matatu kuimarisha sheria katika vituo vya magari. Alisema wenyeviti wanapaswa kuchuka hatua na kuwaonya wahudumu hoa na pia wale wanaotegea kujaza abiria kwa kuzingatia sheria wanapotekeleza kazi yao. 

"Nataka kuwaonya wahudumu wa magari na wengine wote ambao wanatabia ya kuita abiria kwa sauti ya juu wakome kwa kuwa ni kinyume na sheria. Kesi za aina hii zaweza kuzuiwa," alisema Ng'etich. 

Aaron Kinywa, mwenyekiti wa shirika moja la matatu katika kituo cha magari cha Kiambu, alisema kwamba wahudumu wengi wamejipata wakikeuka sheria hii bila ya kujua. Alifafanua kwamba kazi ya kuita abiria ni ngumu na wakati mwingine wao hulazimika kupaza sauti ili kuwaita abiria walio mbali.

Alisema kwamba mashindano ya kujaza magari ndiyo tatizo kuu la kuvunja sheria hiyo kwa kuwa kila mtu hutaka kujaza gari lake. 

Hata hivyo, Kinywa alieleza kuwa wenyekiti wenzake wameleta mbinu mpya ya magari kupanga foleni ili kusiwe na kelele wala mabishano. Alisema kwamba wanakibao wanachoweka juu ya gari ambacho huonyesha abiria gari linalobeba wakati huo.