Wahudumu wa matatu katika eneo la Kikuyu wamepewa onyo kali dhidi ya kubeba abiria kupita kiasi wanafunzi wanaporejea shuleni.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza katika ofisi yake siku ya Jumatano, mkuu wa trafiki katika eneo hilo, Inspekta Elizabeth Wakuloba alisema kwamba wahudumu wa matatu walikuwa na mazoea ya kubeba abiria kupita kiasi hasusan wakati ambapo wanafunzi wanporejea shuleni.

Alisema wahudumu watakaopatikana watashtakiwa vikali kwa kuhatarisha maisha na kutofuata sheria za barabarani.

Inspekta Wakuloba alisema kwamba kitengo cha trafiki kitafanya msako mkali kuhakikisha kuwa usalama unadumishwa wakati huu.

Alisema wengi wa wahudumu wanaweka tamaa ya pesa mbele na kutozingatia usalama wa abiria.

Alifafanua kwamba abiria pia wanafaa kujijali kwa kutokubali kuzipanda matatu zilizojaa kwani hao ndio wanaoendeleza hulka hii miongoni mwa wahudumu wa matatu.

Insekta Wakuloba alisema kwamba wahudumu wa gari itakayopatikana ikikeuka sheria hii watashtakiwa.

Hata hivyo, alisema wale abiria watakao patikana hawana viti na wamekalia vibao ambavyo wahudumu wa matatu wanatumia kuweka katikati ya viti ili abiria akalie watashikwa pia kwa kuendeleza ukeukaji wa sheria za barabarani.

"Wakati huu wanafunzi wanaporejea shuleni, wahudumu huwa na tamaa ya pesa ambayo itawatia mashakani. Natuma onyo kali kwa wahudumu wote wasidhubutu kukeuka sheria za barabarani kwa sababu ya tamaa ya pesa," alisema Inspekta Wakuloba.