Serikali ya Kaunti ya Nyamira imeombwa kushirikiana na serikali kuu ili kujenga Taasisi wakazi wa wadi ya Gesima waliahidiwa na serikali katika eneo la Matutu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea na mwadishi huyu siku ya Jumamosi katika Ofisi yake iliyoko maeneo ya Gesima, mwenyekiti wa taasisi ya Enchoro Peter Minyira aliwaomba wasimamizi wa sekta ya elimu katika ya Kaunti ya Nyamira kushirikiana na serikali kuu ili taasisi ambayo serikali kuu iliwahidi wakazi kujenga katika shamba moja karibu na shule ya msingi ya Matutu imejengwa.

Kulingana na mwenyekiti huyo, eneo bunge la Kitutu Masaba na kaunti ya Nyamira kwa jumla inahitaji taasisi kubwa kama chuo cha ufundi, kwa kuwa kuna vijana wengi ambao wanahitaji kujiunga na taasisi ili kujifunza mbinu mbalimbali za kujiendeleza kimaisha.

Aidha, alisema kuwa taasisi hiyo ikijengwa, wakazi wengi watanufaika kwa kuwa vijana kutoka Nyamira huenda hadi mjini Kisii ili kupata mafunzo hayo.

“Wazazi wengi hupata hawana pesa haswa ya kukondisha nyumba kwa watoto wao wakienda katika mahali pengine, lakini taasisi hii ikijengwa watapata nafasi ya wanao kutoka nyumbani ili kupokezwa mbinu mbalimbali,” alihoji Minyira.

Kwingineko, alisema kuwa serikali ya Kaunti ikishirikiana na kujenga taasisi hiyo, hata taasisi ndogo ya Enchoro itafaidika pakubwa.

Minyira aidha alipongeza wazazi wa shule ya msingi ya Matutu kwa kutoa shamba litakalotumika kwa ujenzi huo.