Wakazi wa mtaa wa Mwembe, Kaunti ya Kisii wameombwa kuzingatia usafi kila kuchao ili kujingika kutokana na kuvamiwa na funza.
Akiongea hii leo, Jumatano na wakazi katika mtaa wa Mwembe eneo bunge la Kitutu Masaba, mhudumu wa afya ya Jamii katika kaunti ya Kisii Kepha King’oina alichukua fursa hiyo na kuwaomba wakazi hao kuzingatia usafi ili kujingika kutoka na funza hao.
“Nawaomba mzingatie usafi na mahali mnamoishi lazima mhakikishe kuwa ni pasafi kila wakati na muwe mnafagia nyumba kwani funza hawa upenda mahali pachafu,” alihoji King’oina.
Aidha, alisema kuwa wao kama wahudumu wa afya wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa funza, ambazo zimekuwa matatizo kwa jamii hazipo tena.
“Tumeweka mikakati kabambe ya kupambana na funza hawa kwani huwa wanasumbua jamii nyingi, nanyi mnastahili kuwajibika wakati funza hawa wamevamia mtu jaribu kuturipoti mapema kabla mtu kuadhiiiwa na funza hawa zaidi,” aliongezea King’oina.
Wakazi wameomba serikali ya kaunti kupitia sekta ya afya kuweka madawa zaidi na kutoa mafunzo jinsi ya kukabiliana na funza hao katika jamii.
“Naomba serikali yetu ya kaunti kushughulikia jambo hili na kuweka pesa zitakazowasaidia wanaothiriwa na funza hawa,” alihoji Beatrice Gesare, mkaazi.