Wakaazi wa eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini, kaunti ya kisii wamemwomba mbunge wa eneo bunge hilo Jimmy Angwenyi kukarabati barabara za eneo hilo sawia na maendeleo mengine jinsi alivyowahidi wakati wa kampeini na hata mapema mwaka jana.
Wakizungumza na huyu mwandishi mnamo siku ya Jumapili katika eneo la Sombogo wadi ya Sensi, wakaazi hao waliokuwa wanaelekea kanisa ya katholiki ya Marani walimwomba mbunge huyo kufanya maendeleo katika eneo hilo haswa ukarabati wa barabara.
“Mbunge wetu alituahidi tukimchagua angetufanyia maendeo na tufurahie uongonzi wake, lakini ni kama ilikuwa kuongea tu maana hatujaona chochote,” alisema Victor Moseti, mkaazi.
Miongoni mwa barabara walizozitaja wanahitaji mbunge huyo kuzikarabati ni kati ya barabara ya kutoka eneo la Mbanda –Marani-Sombogo –Kegogi, ha nyingine ni ya kutoka Nyakoe-Marani, na ile ya kutoka eneo la Itumbe kuuunganisha Kegogi kwa barabara kuu ya Kisii-Eldoret
“Mimi nilimchagua atufanyie maendeleo maana alisema akichaguliwa, kabla ya miaka miwili kukamilika tutaona maendeleo katika eneo hili, haswa kukarabati barabara na shule tunamwomba atimize ahadi,” alihoji Jane Nyakundi, mkaazi mwingine.
Wakati huo huo, wakaazi hao walisema mapema mwaka huu mbunge huyo aliwahidi kuzikarabati barabara hizo kabla ya mwezi wa sita, jambo ambalo walisema hawajaliona likifanywa kamwe.
“Kama anahitaji tufurahie uongonzi wake, wacha afanye maendeleo, tunasumbuka sana mvua inaponyesha, matope yanatusumbua sana,” alidokeza Kevin Nyanga’au, mkaazi mwingine.