Wakaazi wa eneo la Magombo kaunti ya Nyamira wameshukuru serikali ya kaunti na ile ya Kitaifa kwa kuanzisha na kufungua Hospitali mpya katika eneo la Siraati ili kuwahudumia wagonjwa ambao wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne katika eneo la Siraati, wakaazi hao, wakiongonzwa na Benjamin Onkoba walishukuru jitihada za serikali ya Nyamira kwa ushirikiano na serikali ya Kitaifa kuhakikisha kuwa wagonjwa wa eneo hilo wamepata huduma bora ya matibabu.

“Tunasema asante kwa serikali kwa kutufungulia hospitali mpya katika eneo hili ili wagonjwa waweze kuhudumiwa, hayo ndio maendeleo sisi tunahitaji kufanyika katika eneo letu,” alisema Richard Ontiri, mkaazi wa eneo hilo.

Ufungunzi huo wa hospitali hiyo mpya ulifanywa jana na waziri wa afya katika kaunti hiyo Andrew Ombati, jambo ambalo wakaazi hao walifurahishwa nalo.

Wakaazi hao kwa sasa wako na kila sababu ya kutabasamu baada ya kuletewa huduma ya matibabu karibu nao

“Tunaomba serikali iweze kujaza dawa nyingi katika hospitali zetu za hapa kaunti ya Nyamira hii ya Siraati ikiwemo mojawapo ili huduma nayo iweze kuwa ya kuridhisha,” alihoji Evans Omae, mkaazi mwingine.

Hospitali hiyo ilijengwa kupitia pesa za kaunti na zile za hazina ustawi maeneo bunge ya CDF, huku daktari mmoja kwa jina Joyce Onchuru akiletwa katika hospitali hiyo kuwahudumia wagonjwa.