Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa eneo la Nyagesenda, eneo bKnge la Kitutu Chache wametishia kuandamana ikiwa serikali kuu haitawawekea matuta katika barabara la Kegogi –Kisii ili kupunguza idadi ya ajali.

Wakiongea na Mwandishi huyu siku ya Jumapili katika eneo la Masakwe, wengi wa wakaazi hao, wakiongonzwa na Gilbert Osiemo walikiri kuwa barabara zote za eneo hilo zinastahili kuwekwa matuta ili kupunguza mwendo wa magari ambayo huendeshwa kwa kasi na kusababisha ajali kila wakati, huku wakisema wataandama ili serikali isikize kilio chao

Haya yanajiri baada ya mwanamke mmoja kugongwa na gari siku ya Ijumaa katika eneo hilo na kunusurika kifo.

“Tunaomba serikali yetu ikiwa inajali maslahi na maisha yetu kama wananchi wa Kenya ituwekee matuta kwenye barabara zetu haswa hii ya Kegogi –Kisii, la sivyo tuandamane ili wasikie kilio chetu,” alihoji Jared Maina, mkaazi wa Masakwe

“Huenda wananchi wengi kuendelea kugongwa na gari ikiwa serikali haitasikia kilio chetu. Ni jukumu la Serikali kuhakikisha kuwa matuta yamewekwa katika barabara ili ili kupunguza mwendo wa kasi wa magari,” alisema Beatrice Kenani, mkaazi mwingine

Vile vile, Wananchi hao wameongezea kuwa kuna shule nyingi katika sehemu hiyo, na ni mhimu ikiwa watawasaidia kuweka matutu ili kusaidia wanao kuvuka barabara.