Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mkuu wa utamaduni na mila katika kaunti ya Kisii amewaomba wakazi wa kaunti hiyo kutoacha mila na desturi za jamii hiyo.

Akiongea siku ya Jumatano katika wadi ya Gesusu katika hafla ya mazishi ya mwenda zake Mabira Orego, Bwana Obino Nyambane, aliwaomba wakazi hao kuzihifadhi mila na tamaduni za jamii hiyo ili kuzikuza na kuziendeleza kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

“Tume asi mila zetu na kuiga wazungu. Hii ni hatari kubwa sana kwa mila na tamaduni zetu kama jamii ya Wakisii,” alisema Obino.

Aidha, alidokeza kuwa huenda lugha ya Kikisii ikapotea hivi karibuni na kuenea kwa lugha geni katika jamii ya wakisii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwanasiasa Benard Moseti alipongeza serikali kwa juhudi zake za utendakazi na kuse kuwa Raisi Uhuru Kenyatta anafaa kuwapa walimu motisha ili watoe matokeo mema katika mithiani ya taifa

Aliwataka walimu kuwa na subira serikali inaposhughulikia swala hilo ili waafikianae na kurejea kazini.

Mweka hazina wa chama cha Knut tawi la Masaba Kusini Bwana Evans Kalulu, alisema watashikilia msimamo wao na hawatarudi nyuma kamwe hadi pale serikali itakapowajibika kikamilifu.

“Hakuna kurudi nyuma na huu ni mwanzo wa mgomo. Wazazi washirikiane nasi kama wanataka tusaidiane maanake pia sisi ni wazazi,” alisema Kalulu.