Share news tips with us here at Hivisasa

Meneja wa kampuni ya umeme nchini, Kenya Power, mkoani Nyanza Chris Omwenga amewaomba wakaazi wa kaunti ya Kisii kutopanda miti karibu na Nyaya za stima.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa wakati wa kukatwa kwa miti iliyoko karibu na nguzo hizo husababisha maafa kwani huangukia nguzo hizo za stima

Wanaojenga na kuishi karibu na barabara katika ,aunti nzima ya Kisii pia watahitajika kuzingatia sheria za wizara ya ujenzi na barabara na zile za Kampuni ya umeme nchini, Kenya Power wanapopanda miti kando ya barabara.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne mjini Kisii, meneja huyo alisema wakazi waliopanda miti karibu na nguzo za umeme wanaeza pata hasara wakati miti yao itakapoanza kukatwa na kampuni hiyo.

Kulingana na meneja huyo, miti hiyo inapokua huitilafiana na nyaya za stima, hasa wakati wa mvua au upepo mkali, jambo linalosababisha milipuko mara kwa mara.

“Naomba wakazi wote kuzingatia sheria na kutopanda miti karibu na mahala nyaya za stima hupita,”alisema Omwenga.