Share news tips with us here at Hivisasa

Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini imezidi kuwaonya wakazi wanaoishi katika maeneo ya mabonde kuhama ili kuepukana na athari za mvua ya El~Nino inayotarajiwa wakati wowote.

Kulingana na mkurugezi mkuu wa idara hiyo katika kaunti ya Mombasa Lydia Kinoti, Mombasa inatarajiwa kupata viwango ya juu zaidi vya asilimia 90 hadi 95 vya temparecha huku maeneo ya mabonde yakitarajia kushughuhia mvua kubwa zaidi na upepo mkali.

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Kinoti alisema kwamba maeneo ya kisiwani Mombasa yanatarajia viwango vya mvua vya mililita 250 ambayo ni hatari zaidi kwa maisha ya wakazi na huenda yakasababisha madhara ya kiafya kwa wakazi endapo wahatazingatia tahadhari hiyo.

“Iwapo wakaazi hawatazingatia tahadhari tunawaambia basi huenda kukashughudiwa maradhi ya kiafya na makaazi ya wananchi yakasombwa na maji na kusababisha hata maafa. Tungependa kuzingatia hilo na tuhame maeneo ambayo ni mabonde," alisema Kinoti.

Amewataka wakazi wa maeneo ya vitongoji duni vya Moroto eneo la Tudor, Kalahari eneo la Changamwe, Shell beach eneo la Likoni, Kisauni na Mishomoroni kuyahama maeneo hayo ili kuepukana na maporomoko na mafuriko yanapotokea.

Aidha, alisema kwamba wakazi watakaoathiri na mvua hiyo ya elnino wametengewa vituo vya usaidizi katika maeneo ya uwanja wa Tononoka kisiwani Mombasa, ,afisi za wazima moto eneo la Likoni, uwanja wa maonyesho ya kilimo ya Mombasa eneo la Kisauni na shule ya upili ya Kajembe eneo la Changamwe miongoni mwa vituo vingine.

“Tumejiandaa vya kutosha kukabiliana vilivyo na mvua ya elnino pindi itakapoanza kunyesha na wale watakaoathiri pia tumewatengea mahali pakujistiri kwa kipindi ambacho mvua hiyo itakuwa ikinyesha ili kuona kwamba watu wetu wako salama,”aliongeza.

Mvua hiyo ya Elnino inatarajiwa kuanza kunyesha mwezi huu wa Octoba hadi Januari mwaka ujao kulingana na jinsi wanasayani wa idara ya utabiri wa hali ya anga walivyotanga.