Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Baadhi ya wakazi wa Itumbe eneo bunge la Bobasi katika Kaunti ya Kisii wamemuomba Mbunge wao Stephen Manoti kuingilia kati na kuwasaidia kuweka matuta katika barabara ya Kisii-kilgoris.

Wakiongea na Mwadishi huyu siku ya Jumatatu katika soko la Itumbe, wakazi hao walisema kuwa kutokana na ajali nyingi ambazo zimekuwa zikishuhudiwa katika eneo hilo, wanamuomba mbunge huyo kuongea na watu husika ili matuta yawekwe kwenye barabara hilo ili kuzui vifo zaida kutokana na ajali za barabara.

“Namuomba mbunge wetu kuingilia kati swala hili nakuongea na watuhusika ili waweka matuta katika barabara hili kwani ajali zimekuwa zikishuhudiwa kila siku, jambo ambalo ni la kusikitisha miongoni mwa wakazi na wafanyibiashara wa eneo hili," alihoji Justus Nyakweba, Mkazi.

Kwa mujibu wa wakazi hao, mbunge jirani wa Eneo Bunge la Nyaribari Chache alihakikisha kwamba amewasaidia wakazi wa eneo lake kuweka matuta katika sehemu ya Kigoro ambayo yamepunguza visa vya ajali na kumuomba mbunge wao kuiga mfano huo kwa kuhakikisha wameweka matuta hayo barabarani.

Aidha, wamewaomba madereva na wanaoendesha bodaboda kupunguza mwendo ili kuepuka na ajali ya mara kwa mara haswa kwa wanaotumia miguu katika soko hilo huku wakiongojea kushughulikiwa na mbunge huyu.

"Nawaomba wenzangu kutoendesha gari na pikipiki kwa mwendo kasi kwani maafa tumeshuhudia hapa yamekuwa yanasababishwa na gari au pikipiki zinazoendeshwa kwa kasi sana," aliongeza Susan Isoe mkazi mwingine.

Kwingineko, wamewaomba wanaotumia miguu kuwa makini wanapotembea barabarani haswa wakati wanavuka kwenda pande mwingini.