Wakaazi wa Kiamabundu katika wadi ya Kisii ya Kati watanufaika na mradi wa kuwekewa stima bila malipo kutoka kwa wahisani wema.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea na wakazi hiyo siku ya Jumatatu katika eneo hilo, aliyekuwa diwani wa wadi hiyo Kepha Mrefu, ambaye alikuwa na mwakilishi wa wahisani hao, aliwaomba wakazi hao kujaza fomu ili kunufaika na mradi huo.

Kulingana na ratiba ya wahisani hao, kila mkazi atakayenufaika na mradi huo wa stima bila malipo ni lazima nyumba yake iwe karibu na mti wa stima kwani mradi ho utaweka nyaya pekee.

Aidha, Mrefu alitaja kuwa hiyo ni njia mojawapo ya kuleta maendeleo katika wadi hiyo, kwani watu wataweza kufungua biashara mbalimbali na kusema kuwa stima ni muhimu kwa mwanaichi wa kawaida.

“Leo hii tumepata wahisani wema ambao wanataka kutuwekea stima bila Malipo, kwa hivyo nawaomba mjaze hizi fomu ili wapate maelezo yenu kwa njia inayostaili ili muweze kunufaika na mradi huo,” alihoji Mrefu.

Aidha, aliongezea kuwa sehemu zingine katika mji wa Kisii zilinufaika na mradi huo kama maeneo ya Rubia, ambapo Benki ya Dunia kwa ushirikiano na kampuni ya Nguvu za umeme waliwawekea stima wakazi hao mwaka jana.

Baadhi ya wakazi waliojaza fomu hizo waliomba wahisani hao kuwasaidia kwani wakipata stima wataweza kuanzisha biashara.

“Nitafurahia sana nikipata stima kwani nitafungua biashara kama kinyozi ili nami nijiendeleze kimaisha,” alihoji Venna Makori, mkaazi.