Wakazi wa eneo la Kiendege kaunti ya Nyamira siku ya Jumatano walizuia ukarabati wa barabara ya kutoka Kemera – Kiendege kuelekea Nyaneke.
Kulingana na wakazi hao, ukarabati huo unafaa uanzie eneo la Kemera kuelekea Nyaneke, wala si kuanzia eneo la Nyaneke jinsi wanakandarasi walivyoagizwa na mwakilishi wa wadi hiyo James Mating’a .
Jambo hilo lilisababisha vurugu kati ya wanakandarasi na wakazi hao wa Kiendege na wa kemera.
Wakazi hao walizuia magari ya kupeleka mchanga wa kutumika kwa ukarabati huo katika eneo hilo la Kemera na Kiendege, wakihitaji kuona ukarabati wa barabara kuanziwa eneo hilo la Kemera.
Jambo hilo lilimlazimu mwakilishi wa wadi hiyo James Mating’a kuingilia kati na kusimamisha vurugu hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari hiyo jana Jumatano, Matiang’a alisema kulingana na ratiba waliyokuwa nayo, ukurabati unastahili kuanzia eneo la Nyaneke.
“Inaonekena kuwa vurugu hizi ni za kisiasa, wakati niliona wakazi wakisimamisha magari ya mchanga na kuzizuia ni jambo mbaya sana, wangesubiri bora ukarabati ukamilike,” alisema Mating’a.
“Mimi sijawahi ona ukarabati wa barabara ukianziwa nyuma kuja mbele, ujenzi wa barabara unanzia mwanzo kuelekea mwisho na mwanzo ni eneo la Kemera kuelekea Nyaneke wala si kuanzia Nyaneke kuja Kemera,” alisema Peter Mwango, mkazi.