Wakazi wa eneo la Nyamache wamehaidiwa kufaidi kutoka kwa mradi wa serikali wa ugavi wa neti zilizotibiwa ili kujikinga na malaria msimu huu wa mvua.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza katika hafla ya sita ya sherehe za siku ya Mashujaa wa taifa eneo la Nyamache, mkuu wa wilaya hiyo Stanley Too alisema kuwa serikali imetoa vyandarua vya kutosha kwa wote waliosajiliwa.

"Neti zitatolewa kwa waliosajiliwa katika maeneo yaliyoteuliwa na chifu na manaibu wao wataongoza shugli hiyo," Too alisema. 

Haldhalika, alielekeza kuwa wale waliokosa kusajiliwa watashuglikiwa baada ya waliosajiliwa kuhudumiwa. 

Aliwaomba wananchi kutumia neti hizo ipasavyo, huku akiwaarifu kuwa sio za bure bali hununuliwa kwa ushuru wanaoulipa. 

Zoezi hilo limeratibiwa kuzinduliwa tarehe 29 mwezi huu na kuendelezwa kwa siku tano.