Wakazi wa omosocho wadi ya Kisii ya kati wamewaomba wenzao wanaofulia nguo mtoni kuzingatia usafi kama njia moja ya kulinda maji wanayotumia katika eneo hilo.
Wakiongea siku ya Jumanne katika mto wa Omosocho wadi ya Kisii ya Kati eneo bunge la Nyaribari Chache, baadhi ya wakazi waliwalaumu wenzao wanaofulia nguo mtoni kwa kutozingatia usafi kwa kumwaga maji chafu mtoni na kuchafua maji hayo.
Aidha, walisema kuwa ni wajibu wa kila mtu kutunza mazingira haswa maji kwani maji hutumiwa na watu wengi katika shughuli za kila siku.
Wakazi hao walisema kuwa maji yasipokuwa safi huenda watu wakaambukizwa magonjwa, huku wakiwaonya wenzao kutochafua maji hayo na ikiwa wataosheoa nguo zao mtoni, sharti wazingatie usafi.
“Maji ni uhai na hatuwezi kuvumilia tukiona akina mama wengine wakichafu maji haya. Ikiwa hawataki kuwajibika sharti wakome kuja mtoni kuoshea nguo hapa kwani wanatuchafulia maji," alisema Mama Brian.
Muhudumu wa afya ya Jamii katika kaunti ya Kisii Kepha King’oina amewaomba akina mama hao kuzingatia usafi kama njia moja ya kujiepusha na magonjwa yanatokana na maji chafu.
“Nawaomba watu wote kuzingatia usafi haswa wanapotumia maji katika shughuli zao za kila siku ili kujingika na magonjwa mbalimbali," alisema King’oina.
Kulingana na king’oina, akina mama hao wanastahili kuchukuliwa hatua ya kisheri na shirika linalosimamia masuala ya mazingira na kuwaomba kukoma tabia hiyo.
Aidha, alisema kuwa visa vya ugonjwa zinazosababishwa na utumizi wa maji chafu vimeripotiwa katika hospitali ya Kisii huku akiwaomba wakazi kuzingatia usafi na kutumia maji safi.