Wakazi wametakiwa kuwaepusha wanao kutembea kwenye maji ya mvua ambayo yanasababishwa na mvua inayoshuhudiwa katika eneo la pwani.
Msimamamizi wa masuala ya afya katika eneo la Bomu-Likoni Joel Aketch ametoa onyo hilo huku wazazi wengi wakionekana wakiwachukua wano kwenye vituo vya afya kulalamikia kuumwa tumbo na kuendesha.
Afisa huyo wa afya ya umma alisema kuwa ni hatari kubwa inayowakodolea macho wazazi ambao wanawaacha watoto wao kuchezea maji hayo ya mvua ambayo mara nyingi huwa yamechanganyika na maji taka, na kudai kuwa watoto wengi wanapotoka shuleni hujipata wakiyachezea maji hayo hata mpaka wengine huyanywa .
“Maji hayo mara nyingi yanakuwa mseto wa maji ya mvua pamoja na siweji ambayo wakati mvua ikinyesha huwa inavunja mabomba pamoja na miundomsingi ya kudhibiti majitaka kwenye majengo pamoja na viwanda vilivyomo katika mji huu wa Mombasa,” alisema afisa huyo.
Aliwataka wazazi kuwanunulia wanao nguo na viatu ambavyo vitawasaidia kutogusana na maji hayo machafu kwa urahisi, na kuwasihi kuwajibikia wanao hasa nyakati wanatoka shuleni na kuwakanya kutembea njea wakiwa bila viatu.
“Ni salama watoto kununuliwa vyatu virefu ambavyo vitawafaa kwenye msimu huu wa mvua nyingi na kujizuia dhidi ya kupata maradhi yanayotokana na maji taka au viini vya maji kwa jumla,” alisema daktari huyo.