Wakazi na wafanyibiashara wilayani Kenyenya, eneo bunge la Bomachoge Borabu wamekashfu kampuni ya nguvu za umeme nchini KPLC kwa hitilafu za umeme kwa siku ya tano mfululizo.
Wakiongea na waandishi wa habari siku ya Jumatano wilayani kenyenya, wakazai hao, wakiongozwa na Cleophas mose walisema eneo hilo limekosa nguvu za umeme kwa siku ya tano mfululizo, huku zikija na kuenda kila wakati na kuwasababishia hasara kubwa kwani wengi wao wanategemea nguvu za umeme kwa bishara yao.
“Mimi ni fundi wa kutengeneza dirisha na milango ya chuma, wakati nguvu za umeme zimekosekana, biashara yangu husimama kwa muda mpaka nitafute njia mbadala ili kumalizia wateja wangu kazi zao na huwa hasara kwangu,” alihoji Victor Mogaka, fundi.
Aidha, fundi huyo aliongezea kuwa anapotumia njia mbadala, hatengezi pesa inavyostahili kwani anapata faida ndogo ikilinganishwa na wakati anatumia umeme.
“Kutumia kifaa kama vile genereta ni ghali mno kwangu, maana hutumia petroli nyingi na huwa gharama kwangu, naomba kampuni ya KPLC itukumbuke kama wanabiashara na kutuonyesha uwazi maana tunawalipa baada ya kutumia nguvu hizo,” aliongezea Mogaka.
“Inabidi ninaabiri pikipiki kuenda kununua petroli wakati nguvu za umeme haziko na nauli hiyo natumia kuleta mafuta tena ni hasara maana stima ingekuwa singepoteza hizo pesa," aliongezea.
wakati huo huo, wakaazi wengine walikiri kuwa mawasiliano yao hukatizwa kwa ghafla, maana simu zinapoisha moto hakuna mbinu mbadala, jambo ambalo wamekerwa nalo na kuomba kampuni ya umeme kulishughulikia kikamilifu na kujali maslahi ya wakenya wote kwa usawa.