Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakazi wa eneo bunge la Bomachoge borabu katika kaunti ya Kisii waliandamana kulalamikia kutofanywa kwa maendeleo katika eneo hilo.

Maandanamo hayo yalishuhudiwa siku ya Jumatano katika eneo bunge hilo, huku wakiapa kuwa hawatatozwa ushuru hadi gavana wa kaunti hiyo Jame Ongwae awafanyie maendeleo katika eneo bunge hilo.

Waandamanaji hao waliwafurusha watoza ushuru kutoka soko ya Kenyenya na Mogonga, na kusema hawataruhusiwa kukusanya ushuru katika eneo hilo hadi waone maendeleo yanafanywa katika eneo hilo.

Miongoni mwa maenmdeleo wanayoyahitaji ni ukarabati wa masoko, barabara za eneo bunge hilo, kutengenezwa kwa vyoo safi katika soko za eneo hilo, kutobaguliwa katika nafasi za ajira katika kaunti ya Kisii na miongoni mwa mengine .

Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Mogonga, waandamanaji hao, wakiongozwa na Douglas Onsase walikiri kuwa kuna baadhi ya watu walioenda kwa ofisi ya gavana kulalamikia kutofanywa kwa maendeleo katika eneo hilo, kisha wakapokezwa shillingi laki mbili ili kuwanyamanzisha,  na baadaye wakaona eneo bunge nzima halitakubali kuuzwa kwa pesa hizo.

“Serikali ilitoa shillingi 200,000 ili kutunyamanzisha, na baadhi yetu tulipokezwa 2,000 kila mmoja na tukaona haiwezekani tuuze eneo bunge letu kwa pesa hizo, kile tunahitaji ni maendeleo katika eneo bunge letu,” alisema Cleophas Nyakoe, mkazi.