Wakenya kote nchini wameombwa kuungana pamoja kusaidia kupambana na changamoto zinazowakumba kama njia mojawapo ya kustawisha nchi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akisoma hotuba ya mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta wakati wa sherehe ya mashujaa uwanjani 64 siku ya Jumanne, kamishna wa Kaunti ya Uasin Gishu Abdi Hassan, aliwaomba vijana kuungana kuleta maendeleo badala ya kutenganishwa na wanasiasa.

"Tunawaomba Wakenya wawe na mwito mmoja wa uwiano na utangamano na kufanya kazi pamoja kwa kutilia maani maadili ya kijamiii. Bila kutenganishwa tutaendelea mbele," ilisema hotuba hiyo.

Aidha, Hassan aliwaomba wakazi wa Uasin Gishu kuwatambua wahalifu wanaowasumbua kwa kuleta utovu wa usalama.

"Nawaomba mutupashe habari kuhusu uhalifu ili maafisa wa usalama wakabiliane nao vilivyo. Mukifanya hivyo, nawahakikishia usalama utaimarishwa,” alisema Hassan.