Share news tips with us here at Hivisasa

Wanaume wawili wamefikishwa mbele ya mahakama moja hapa mjini Nakuru, kujibu shtaka la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka kumi.

Washtakiwa hao Mureithi Ngari wa miaka 80 na Tom Mungai wa miaka 85 wanakisiwa kutenda kitendo hicho tarehe Juni 16, 2015 katika kijiji cha Tangitano, wilaya ya Gilgil katika jimbo la Nakuru.

Akitoa ushahidi wake mama mtoto huyo alimwambia hakimu mkuu Doreen Mulekyo Kwamba bintiye alirejea nyumbani aklia na kumueleza kilichotokea kabla ya mama huyo kumpeleka hospitali ya Gilgil ilikobainiwa kwamba alikuwa amenajisiwa.

“Alirejea nyumbani Jioni akitoka shule huku akitokwa na machozi na kunihadithia kilichojiri,” alisema mama huyo.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kumpa msichana huyo chakula kilichokuwa na madawa ya kuongeza usingizi alipokuwa akitoka shuleni kabla ya kumfanyia kitendo hicho.

Wakijitetea mbele ya mahakama hayo, washtakiwa hao walikanusha madai hayo na kuyataja kama yasiyokuwa ya kweli huku wakisema kwamba umri wao hauwaruhusu kufanya kitendo kama hiko.

Hakimu huyo amesema kwamba ni kinyume na sheria na aibu kubwa mno kwa watu wazima haswa wenye umri mkubwa kama huo kumtendea binti mdogo uhalifu kama huo akiongeza kwamba iwapo washtakiwa hao watapatikana na hatia, watakuwa kielelezo chema kwa wahalifu wengine.

Washukiwa hao wameachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000 kila mmoja na kesi hiyo itasikilizwa tarehe 24 mwezi huu.