Share news tips with us here at Hivisasa

Kanisa zote nchini zimeombwa kuwa katika mstari wa mbele kuwafunza vijana kuwa na madili mema katika Jamii, haswa katika vyuo mbalimbali na taasisi zote kama njia moja ya kuwaepusha na maovu katika shule hizo.

Akiongea siku ya Jumapili katika Kanisa la Kisii PAG lililoko mjini Kisii, mwenyekiti wa shirika la Biblia za Gideons Brother Gideon aliwaomba wakirsto wote kushirikiana ili kuwafunza vijana madili mema, ili kizazi hiki kiwe cha manufaa kwa nchi ya Kenya.

Aidha, alisema ni kupitia kanisa ambapo nchi zitaweza kuwa na Amani, kwani wakristio wana jukumu kubwa la kuombea nchi kuwa na amni kupitia kuwa na mafunzo kwa Jamii.

“Sisi wakirsto tuko na nafsi kubwa katika taifa letu, kwa hivyo ni wajibu wetu kuhubiri amani miongoni mwa wakenya kama njia moja ya kuinua viwango vya nchi yetu,” alihoji Gideon

Brother Gideon alisema kuwa kupitia shirika la bibilia za Gideons, vijana wengi wamepata funzo maalumu jinsi ya kujiepusha na mambo ya ugaidi, jambo ambalo alisema kuwa wakristo wanastahili kuzingatia sana.

Kwingineko, aliwaomba wakiristo wote kushirikiana na shirika la Biblia za Gideons ili kueneza injili katika kila upande wa nchi.