Wakulima wa mahindi katika kaunti ya Kisii wameshauriwa kutumia gunia ambazo zimetengenezwa kupitia mfumo wa teknolojia ya kisasa wakati wanapoweka mahindi yao ili kutunza mahidi hayo bila kuvahamiwa na wadudu kama njia moja ya kupunguza janga la njaa katika kaunti hiyo.
Gunia hizo za kisasa zimetengenezwa zikiwa na makaratasi mawili kutoka ndani kisha gunia yenyewe ikiwa kutoka nje, gunia ambazo zinasemekana kutunza mahindi bila kuvahamiwa na wadudu na kutotumia dawa yoyote.
Akiongea na waandishi wa habari mnamo siku ya Jumapili mjini Kisii, afisa wa chama cha United States Agency for International Development katika kaunti ya Kisii Yobesh Onyancha aliwaomba wakulima kutumia gunia hizo za kisasa wanapoyaweka mahindi yao ili kutoaribiwa na wadudu.
Hii ni baada ya idadi nyingi ya wakulima katika kaunti ya Kisii kuwa na changamoto nyingi wanapoweka mahindi yao kwa kuvahamiwa na wadudu, huku akisema wakati wakulima wanapotumia dawa kuwaangamiza wadudu hao dawa hiyo husababisha madhara kwa binadamu haswa kwa tumbo, jambo ambalo lilipelekea chama hicho cha USAID kutengeneza gunia hizo za kisasa.
“Tunawahimiza wakulima wa mahindi kutumia gunia maalumu, gunia ambazo zitatunza mahindi bila kutuma dawa ambayo inawasumbua binadamu kwa kuumwa kwa tumbo. Gunia hizi zitasaidia pakubwa na zimetibithishwa kuwa nzuri,” alisema Onyancha.