Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakulima katika kaunti ya Uasin Gishu wamehimizwa kutunza vizuri kumbukumbu zao ya kilimo ili kuzitumia katika siku za usoni.

Akizungumza afisini mwake siku ya Jumanne, waziri wa kilimo katika kaunti hiyo Cyril Cheruiyot alisema kuwa utunzaji wa kumbukumbu hizo zitawasaidia kujua ikiwa wanapata faida ama hasara.

“Kilimo kitakuwa kinadidimia kila siku ikiwa mkulima hatatunza kumbukumbu ya jinsi anavyotumia vitu kama dawa, mbolea na megine mengi,” alisema Cheruiyot.

Cheroiyot aliongeza kuwa kumbukumbu hizo aidha, zitamwepusha mkulima kutokana na madeni kwani atakuwa anaandika jinsi uuzaji unaendelea.

Waziri huyo aidha aliwaomba wakulima kujiunga na makundi ambayo yatawawezesha kupata mikopo ya kukuza kilimo.

Alisisitiza kuwa ikiwa wakulima watajiunga na vikundi hivyo, serikali itawasaidia na kuwawezesha kupata vitu kama vile mbolea kwa bei nafuu.