Mkulima mmoja kutoka Gusii amewaomba wakulima kutoka eneo la Nyanza kuanzisha ufugaji wa nyuki kuinua kilimo cha kila aina katika eneo hilo.
Akiongea hii leo Jumamosi katika maonyesho ya kilimo na biashara ambayo yanaendelea katika uwanja wa Gusii, katika Kaunti ya Kisii, mkulima Samson Nyamweya aliwahimiza wakulima kuanzisha ufugaji wa nyuki katika maeneo yote ya Kaunti ya Nyamira, Kisii na Migori kwani asali ni dawa kwa binadamu.
“Nawaomba wakulima kufuga nyuki kwa kuwa nyuki ni faida kubwa kwa kilimo na utoa asali ambyo ni dawa kwa binadamu,” alisema mkulima Nyamweya.
Kwa mujibu wa Nyamweya, ufugaji wa nyuki ni aina moja ya kilimo na mkulima ataweza kujiendeleza kwani nyuki hutoa asali ambayo mkulima ataweza kuuza na kupata kile anachohitaji.
Aidha, alisema kuwa watu wengi uogopa kufuga nyuki kwa kile wanasema kuwa wataweza kuwashambulia watu wa jamii au wanyama wengine katika boma.
Nyamweya alikanusha madai ya wakulima kuwa nyuki hushambulia watu na kusema nyuki ni kiumbe ambaye anafahamu vyema mkulima wake bora mkulima awatunze kufuatiana na masharti ya kuwafuga.
Kwingineko alisema kuwa nyuki huchangia mimea mingine kumea na wakulima wengine kupata chakula kwani nyuki husaidia kubeba mwenge kutoka kwa mmea hadi nyingine ndiposa mimea hiyo inakuwa na kutoa chakula.
Kwa sasa Nyamweya amewaomba wakazi hao kuzingatia mafunzo yote wanayopata kutoka kwa maonyesho ya mwaka huu ili waweze kuinua kilimo katika eneo la Nyanza.
“Nawaomba wakulima wote kuzingatia mafundisho haya muhimu ili tuweze kuinia kilimo chetu katika eneo hili la Nyanza," alihoji Nyamweya.