Katibu wa chama cha Knut tawi la Nyamira, Nicholas Nyang’au, amewaomba walimu kutoasi mgomo wa walimu na kuendelea na mgomo huo hadi watakapopata haki ya kuongezewa mshahara wao.
Nyang’au alisema wiki hii ya tatu ya mgomo huo itakuwa na maandamano makubwa ambayo hayajawahi shuhudiwa nchini ili kushinikiza serikali kuwaongezea mshahara na kufuata uamuzi wa mahakama.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumapili katika mji wa Nyamira, Nyang’au aliwaomba walimu kuendelea kushirikiana kwa mgomo.
“Tumeingia awamu ya tatu wa mgomo na hakuna yeyote atatisha walimu. Tutaendelea na maandamano makubwa hadi tupate haki yetu,” alisema Nyang’au.
Aliongezea: “Naomba walimu msiwe mnatatanishwa na kutishwa na yeyote. Sisi kama walimu tutaendelea kusimama imara na ni lazima tupate haki yetu jinsi mahakama kuu ilivyoagiza na hakuna mwalimu ataingia darasan ikiwa hatujalipwa nyongeza yetu ya mshara.”
Wazazi na walimu wameoimba serikali kuu kuwaongeza walimu pesa ili kurejelea shuleni kwani mitihani ya darasa la nane na kidato cha nne iko karibu kuanza.