Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Licha ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne kuanza siku ya Jumatatu bila tashwishwi lolote, walimu wametishia kuishtaki tume ya kuajiri walimu, TSC, kwa kukosa kuwalipa mishahara ya mwezi Septemba.

Muungano wa walimu nchini Knut, unatarajiwa kufanya mazungumzo na wakili wake ili kupata suluhu kuhusiana na mishahara, huku muungano wa Kuppet ikipanga kupeleka malalamishi yake kortini kustaki tume ya kuwaajiri walimu iwapo mishahara haitalipwa ifikapo siku ya Jumatatu.

Wakati wa mgomo, tume ya TSC ilikuwa imewaonya walimu ambao hawatafika kazini kuanzia tarehe 18 mwezi Septemba watafutwa kazi.

Mahakama kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wake tarehe 6 mwezi Novemba, hususan ikiwa nyongeza ya mishahara ambayo walimu wanadai ilikuwa ya halali au la.

Walimu walirejea kazini tarehe tano mwezi huu kufuatia agizo la mahakama, huku mgogoro kuhusiana na malipo ya mwezi Septemba ukiwa bado unaendelea.