Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Chama cha waadventista chawania kuanzisha ufugaji wa mbuzi wa maziwa katika Wadi ya Gesusu, Kaunti ya Kisii hivi karibuni.

Wakiongozwa na katibu wao Bonuke Zabron, wanachama hao waliahidi kutatua ukosefu wa maziwa ya mbuzi katika eneo hilo na katika kaunti nzima ya kisii.

Wakiongea katika maeneo ya Riochungo siku ya Alhamisi wakiwa katika harakati za kutafuta ushauri kutoka kwa daktari wa mifugo Bwana James Onchagwa ambaye pia ni mwalimu wa maswala ya ufugaji wa mifugo, walisema kuwa kaunti hiyo ikona uhaba wa maziwa ya mbuzi.

"Tume tambua ya kwamba maziwa ya mbuzi hayapatikani kwa urahisi katika maeneo ya Kisii. Tumechukua hatua hii ili kuhakikisha maeneo haya yetu yana maziwa ya mbuzi," alisema Bonuke.

Daktari Onchagwa aliwapongeza wafugaji wa kundi hicho na kuahidi kushirikiana nao hili kuimarisha ufugaji wa mbuzi wa kutoa maziwa katika jamii na taifa letu la Kenya.

"Nimefurahia sana kwa hatua yenu na natumai pia makundi mengine ya jamii yetu wataiga mfano wenu ili tuwe tunazalisha maziwa kwa wingi. Kumbuka maziwa ya mbuzi yana manufaa mengi sana kwa maisha na afya zetu kama binadamu," alisema daktari Onchagwa.

Aidha, aliwaarifu wakaazi wa wadi hiyo kuwa maziwa ya mbuzi yana madini ambayo yana umuhimu mkubwa kwa wale wanaougua ugonjwa wa ukimwi na kuwataka wafuge mbuzi ili waweze kunufaika na maziwa hayo.

Aliahidi kuwa atakua akiwatembelea mara kwa mara ili kuhakikisha mbuzi hao wako na afya nzuri.