Wanafunzi wengi wa chuo kikuu cha Maseno wamelalamikia hali ya usafi wa vyoo vya nyumba walizopangisha eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Baadhi yao wamesema kuwa wamiliki wengi wa nyumba za kupangisha hawatilii maanani usafi wa vyoo pale wanapoamua kujenga nyumba za kupangisha.

Maeneo ya Posta, hali mbaya ya vyoo huwa fondogoo ndiyo hukaribishaji wanaotembea huko. Hapa, wanafunzi wanaoishi kwenye nyumba za kupanga walilalamikia hali hiyo na kusema kuwa hawangelipa fedha wanazoitishwa na mmiliki wa nyumba hizo kikamilifu iwapo hali hiyo haitarekebishwa.

"Landlord wetu tunamtafuta hatumwoni na choo zimejaa," alisema Laurine, mwanafunzi mmoja na ambaye pia ni mpangaji wa nyumba maeneo hayo.

Juhudi zetu za kutaka kuzungumza na mmiliki wa nyumba hizo Charles Kuya ziligonga mwamba baada ya simu yake kuwa imezimwa na hatimaye alipopatikana, Kuya alisema kuwa nyumba zile si zake bali ni za mkewe na hivyo basi hangelizungumzia swala hilo.

Hali hii duni inachangiwa na kuwepo kwa uhaba wa nyumba za kupangisha eneo hilo huku wanafunzi wengi wakilazimika kuishi zaidi ya wawili katika vyumba vyenye nafasi ndogo.

Wanafunzi hao sasa wametoa wito kwa usimamizi wa chuo kikuu cha Maseno kufanya kazi pamoja na wamiliki wa nyumba hizo ili kuhakikisha kuwa huduma wanazozipata wanafunzi hao zinaboreshwa na pia gharama ya kulipa nyumba hizo kudhibitiwa ili kupunguza visa vya wamiliki hao kuongeza kodi zao kila uchao.