Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi wa wadi ya Menengai kwenye Kaunti ya Nakuru Michael Macharia, amewataka watahiniwa wa mithani wa kitaifa wa kidato cha nne kutotumia njia za mkato kupitia mitihani yao ya kitaifa.

Akizungumza kwenye shule ya upili ya Upper Hill Nakuru siku ya Alhamisi, Macharia aliwahimiza wanafunzi hao kutegemea elimu waliyo nayo ili kupitia mtihani huo na pia kumtumainia Mungu.

Mwakilishi huyo wa wadi aliangazia tukio ambalo mwanafunzi mmoja alitegemea njia ya mkato almaarufu ‘mwakenya’ kuptia mtihani wake wa kitaifa hatua iliyompelekea kujipata taabani.

‘Mmoja wa wanafunzi aliyekuwa katika shule hii alikuwa akifanya vyema kwenye mitihani yake ya kawaida na baada ya kuwepo kwa fununu kuhusiana na baadhi ya yaliyomo kwenye mtihani huo, aliamua kutegemea hilo na baada yake kuingia kwenye chumba cha mitihani, hakuamni macho yake kwani vidokezo walivyokuwa wamepata havikuwa sahihi,” alisema Macharia.

Kwa sasa, wanafunzi wengi wa shule za umma kote nchini wanaendelea kujisomesha kwa kukosa wa kuwafunza kufuatia mgomo wa walimu ambao unashuhudiwa kote nchini.

Wanafunzi wamelazimika kubuni njia mpya za kuendelea na masomo huku wanafunzi wengi wa mjini Nakuru wakifurika kwenye maktaba ya kitaifa iliyo Nakuru kujisomea.