Wanaochoma mahindi katika mji wa Kisii wameonywa dhidi ya kuchafua mazingira katika mji huo, na badala yake kuombwa kutunza mazingira.
Akiongea na baadhi ya wanabiashara hao siku ya Jumanne katika mji wa Kisii, mwenyekiti wa kikundi cha Muungano Minto Youth Kepha King’oina, wanabiashara hao waliombwa kutunza mazingira ili kuinua viwango vya usafi wa mji huo.
King’goina alisema kuwa imekuwa mazoea ya wengi kutojali mahali pa kutupa uchafu, bora tu yeye afanye biashara na kuenda zake bila kukumbuka kuwa keshoye watataka mahala hapo pawe pasafi ili kuvutia wateja.
“Nawaomba wafanyabiashara wote kuzingatia usafi na kutotupa uchafu kiholelaholela ili tuweze kushirikiana pamoja kuinua viwangio vya usafi,” aliseam King’oina.
Kwa sasa, wafanyibiashara hao wameombwa kuwajibika na kuhakikisha kuwa mahali popote wanapofanyia biashara ni pasafi kila wakati; haswa wanaofanyia biashara zao karibu na duka kandokando mwa barabara.
Kulingana na mwenyekiti huyo, kuna baadhi ya wanabiashara wanaotupa uchafu huo kimakusudi kwa sababu ya kuwa na wafanyikazi wa kufagia mji huo bila kukumbuka kuwa uchafu huo ni hatari kwa afya.
Kwingineko, King’goina aliwaomba wakaazi wote kutumia pipa za kukusanya uchafu ambazo zimewekwa kila sehemu ya mji huo kwa kuweka uchafu wao ili kutunza mazingira ya mji huo.