Jamii ya watu wanaoishi na ulemavu katika eneo la Pwani ya Kenya wamezitaka serikali za kaunti kubuni nafasi za lugha ishara katika afisi za umma.
Katika mahojiano na waandishi wa habari mjini Mombasa siku ya Jamatano, mshirikishi mkuu wa jamii hiyo eneo la Pwani Hamisa Zajja amesema kuwa kutokana na changamoto nyingi jamii hiyo inazopitia wanapotafuta msaada katika afisi za umma kumechangia kuenea kwa dhulma za kijinsia.
Kiongozi huyo amedai kuwa kutokana na ukosefu wa watafsiri wa lugha ishara katika afisi za umma kumechangia kushughudiwa kwa changamoto nyingi huku jamii hiyo ikionekna kutengwa hata bada ya katiba kuangazia haki zao.
“Ni wakati wa viongozi wa serikali kumjumisha mlemavu kama kiungamo muhumi katika ugatuzi iwapo wanazingatia demkrasia ya nchi la sivyo hakuna mtu atahisi kuwepo kwa ugatuzi mashinani na serikali zote za ugatuzi nchini Kenya hazingeandika mtu yoyote wakati huu kama hana masomo ya lugha ishara”, alisema Hamisa.
Hamisa amehoji kuwa ni vyema iwapo serikali za kaunti zitawajiri walemavu katika afisi za umma na kusaidia kurahisisha shughuli za kikazi katika idara mbalimbali za umma kama njia moja wapo ya kuwasaidia walemamu.
Jamii hiyo ya walemavu awali ilidai kutengwa na kunyanyaswa haki zao kikatiba na baadhi ya maafisa wa umma kwani wengi wao husema hufurushwa katika afisin hizo wanpozitembelea hatua ambayo imepelekea kiongozi huyo kuzishinikiza afisi hizo kuajiri watafsiri wa lugha ishara.
“Sio vyema kwa jamii hiyo kutengwa wala kufurushwa wanapozuru katika afisi za umma kutokana hali yao ya kimaumbele na lazima jamii hiyo itambuliwe kama jamii nyingine nchini kwani kila mkenya ana haki kikatiba,” aliongeza Hamisa.
Mapendekezo ya mshirikishi huyo mkuu yamejiri baada ya jamii hiyo kulalamikia kubaguliwa na baadhi ya maafisa wa umma katika idara mbalimbali za serikali wakati wanapozuru katika afisi hizo kutafuta usaidizi wa kiserikali.