Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa Nyamira wanaougua ugonjwa wa figo na ugonjwa wa mifupa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya wataalamu wa magonjwa hayo kufika katika kaunti hiyo ili kuwapa matibabu.

Wataalamu hao kutoka nchi ya CZeck Republic walifika katika kaunti hiyo siku ya Alhamisi wakiwa na nia ya kuwatibu wakazi wambao wameathirika na magonjwa hayo.

Akizungumza siku ya Alhamisi mjini Nyamira, mwenyekiti wa wataalamu hao Fred Milano alisema watashirikiana na maafisa wa afya wa kaunti hiyo kuhakikisha wakazi wanahudumiwa kwa magonjwa hayo kikamilifu.

Afisa mkuu wa matibabu katika hospitali ya Nyamira Level Five Douglas Bosire pamoja ma msimammizi wa hospitali ya Nyamira Daktari Cyrus Ayunga walisema wamekuwa wakipata changamoto chungu nzima ya kuwatibu wale wameathirika na magonjwa ya aina hiyo katika kaunti ya Nyamira.

Ayunga alipongeza wataalamu hao kwa kutembelea Kaunti ya Nyamira na kupongeza chama cha Nadra Kenya kwa kufanya juhudi za kuwafikisha wataalamu hao katika kaunti hiyo.

“Tuko na furaha kwani wale wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa hayo watapata tiba kupitia wataalamu hawa ambao wamefika hapa,” alisema Bosira.

Wale wanaoathiriwa na magonjwa ya figo na mifupa wamealikwa kupata matibabu na kuhudumiwa kikamilifu katika Kaunti ya Nyamira kuanzia juma lijalo.