Wagonjwa wanao ugua ugonjwa wa kifua kikuu katika Kaunti ya Kisii wameombwa kutumia dawa wanayopewa kutoka kwa hospitali kulingana na maagizo na masharti kutoka kwa daktari kama njia moja ya kuwasadia kupona kutoka kwa maradhi hayo.
Akiongea siku ya Jumatatu na wagonjwa hao katika hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii mhudumu wa afya ya Jamii katika Kaunti ya Kisii kepha King’oina aliwaomba wagonjwa hao wawe wakitumia dawa jinzi wamepewa maagizo na masharti kutoka kwa daktari kama njia mojawapo ya kupona na kukinga watu na jamaa zao nkutokana na maambukizi.
Kulingana na mhudumu huyo watu wengi wanaougua ugonjwa wa kifua kikuu wanaporuhusiwa kuenda nyumbani wengi wao huwa hawafuati maagizo ya daktari jambo linalowafanya kuwa wagonjwa zaidi na kuambukiza jamaa zao.
"Nawaomba mkienda nyumbani muwe mnatumia dawa hizi kulingana na maagizo ya daktari ndiposa mpone," alisema Kepha.
Wagonjwa hao ambao wamekuwa hospitalini kwa miezi miwili sasa wamepata nafuu na kuruhusiwa kwenda nyumbani ili waweze kuendelea kutumia madawa wakiwa nyumbani.
Aidha, aliomba jamaa na marafiki wa wagonjwa hao kuwakubali katika Jamii kwani ni ugonjwa ambao una tiba ikiwa mtu atatumia madawa vizuri kulingana na maagizo ya daktari.
"Nawaomba jamaa na marafiki wa wagonjwa wote kuwawakubali katikla Jamii na kuwasadia popote wanapohitaji msaada ili waweze kujiendeleza kimaisha.