Watu wanne waliaga dunia, baada ya ajali ya barabarani iliyotokea katika barabara kuu ya kutoka Kisii kuenda Kilgoris katika eneo la ogembo siku ya Jumapilli.
Ajali hiyo illiyotokea mwendo wa jioni ilitendeka baada ya trekta moja la kukarabati barabara kupoteza mwelekeo na kuwagonga watu waliokuwa katika kituo cha Abiria wakiabiri gari aina ya Nissan, kwenye matatu iliyokua ikipanga kuenda mjini Kisii.
Kulingana na Bwana Samson Omboga, ambaye ni mmoja wa madereva na aliweza kushuhudia ajali hiyo, trekta hiyo ilikuwa na mbio kutoka upande wa Tendere, kabla ya kupoteza mwelekeo na kuwagonga Abiria hao waliokua wakisubiri gari.
Hata hivyo, polisi waliwasili na kuwasaidia manusura, huku wakianzisha uchunguzi wa kilichosababisha ajali hiyo, na kasha baadaye watato ripoti rasmi kuhusiana na kisa hicho.
Wanne hao waliondolewa na kupelekwa katika hifadhi ya wafu ya Kisii Level 6, huku wale waliopata majeraha wakipelekwa hospitali ya Ogembo na wengine ile ya Kisii.
Eneo hilo limeshuhudia ajali nyingi katika siku za hivi majuzi, huku wengi wa Wananchi wakihusisha visa hivyo na mteremko mkubwa ulioko katika eneo hilo.