Share news tips with us here at Hivisasa

Wanafunzi wanaofanya mitihani ya kitaifa ya KCSE mjini Mombasa wameonywa dhidi ya kujihusisha na udanganyifu kwani hatua kali zitachukuliwa kwa watakaopatikana.

Akitoa onyo hilo mjini Mombasa siku ya Jumatatu, Mwalimu mkuu wa Shule ya Upili ya Coast Girls iliyoko mjini Mombasa Khadija Said alisema kwamba wanafanzi watakaopatikana wakishiriki udanganyifu watahadhibiwa kisheria.

Khadija alisema kwamba tayari maafisa wa polisi wanaendeleza doria katika maeneo yaliyotengwa kufanywa mitihani hiyo huku akidhihirisha matumaini yake kuwa wanafunzi hao watafanya vyema zaidi mwaka huu.

Aidha, alisema kwamba wanafunzi wamejiandaa vyema kwa mitihani hiyo licha ya walimu kote nchini kushiriki mgomo uliyomudu kwa kipindi cha mwezi mmoja na akisema kwamba wanatarajia kuibuka na ushindi baada ya matokea ya mitihani ya mwaka huu kutangazwa mwaka ujao.

“Tungependa kuwaonya wnafunzi wetu kwamba wasijaribu kudanganywa na baadhi ya watu flani na kutumia mitihani ya uongo na kushiriki udanganyifu hiyo sisi hatutakubali, na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaopatikana wakishiriki udanganyifu,” alisema Khadija.