Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Watu watatu waliokuwa wakisafiri kwa pikipiki wamefariki papo hapo katika eneo la Kijipwa kwenye barabara ya Mombasa-Malindi baada ya pikipiki yao kugongana ana kwa ana na lori.

Watatu hao ambao ni wanaume walikumbana na mauti yao baada ya mwendeshaji pikipiki kujaribu kulipita lori ambalo lilikuwa likielekea jijini Mombasa na kukumbana na lori lengine ambalo lilikuwa likielekea Kilifi hapo jana.

Kamanda wa polisi kaunti ya Kilifi Douglas Kanja alieleza kuwa lori lililotekeleza mauaji hayo lilitoweka na kwa sasa maafisa wa polisi wanaendelea kulisaka.

“Waendeshaji pikipiki na madereva wa magari kuweni makini wakati mnapokuwa barabarani ili kupunguza ajali,” alisema Kanja

Miili ya watatu hao inahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya kaunti ya Kilifi.