Wawaklilishi wa wadi katika Kaunti ya Nyamira wanahitajika kurejesha pesa walizopokea kama marupurupu ya vikao na uchukuzi walipokuwa likozoni bila kuwa na kikao ilivyotakiwa kisheria.
Wawakilishi hao wa wadi na Wabunge wanastahili kupokea marupurupu ya vikao na ya uchukuzi wakati wanapohudhuria vikao hivyo bungeni na kusafiri kikazi.
Mfanyi hesabu ya pesa za kaunti al maarufu auditor general Edward Ouko alitoa ripoti ya Kaunti ya Nyamira siku ya Jumatano iliyoonyesha kuwa Wawakilishi hao walikuwa wakipata marupurupu ya vikao wakati walikuwa likizoni pamoja na ya uchukuzi kinyume na sheria.
Pia imebainika kuwa Wawakilishi hao wanakabidhiwa pesa nyingi za uchukuzi wakidanganya kuwa wanaishi mbali na ofisi zao zilizoko Kaunti ya Nyamira ilhali wanaishi karibu na ofisi hizo.
Hayo yote ni kwa majibu wa ripoti ya Ouko aliyesema pesa hizo Wawakilishi wamekuwa wakizichukua bila kufanya kazi akisisitiza kuwa wanastahili kuzirudisha kwa hazina ya serikali ili zifanye maendeleo na kuonyesha haki kwa wananchi wa kaunti hiyo ya Nyamira.
Ripoti ya Ouko inaonyesha Kaunti ya Nyamira ni miongoni mwa kaunti ambazo zilitumia pesa vibaya zaidi.