Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Mugirango Kusini Manson Nyamweya amewakosoa wawakilishi wa wadi katika kaunti ya Kisii kwa kutowajibikia kazi yao vilivyo.

Kulingana na mbunge huyo wawakilishi wa kaunti hiyo wamerudisha maendeleo nyuma kwa kutofuatilia miradi ya maendeleo jinsi inastahili kufanywa katika eneo wanazoziwakilisha.

Akizungumza siku ya Alhamishi kwa hafla ya mazishi yaliyoandaliwa katika eneo la Tendere, Bomachoge Borabu, Nyamweya aliwakosoa wawakilishi hao na kuwashauri kutumikia wananchi vilivyo kwani walichaguliwa kuleta maendeleo.

Aidha, Nyamweya amewaomba wawakilishi hao wa wadi kutumia pesa za wananchi vizuri katika maendeo ili kutimiza ahadi zote walizotoa wakati walikuwa wanatafuta kura kutoka kwa wananchi.

“Waliorudisha kaunti hii nyuma kimaendeleo ni wawakilishi wa wadi. Sionoi kama wawakilshi hawa watatusaidia maana hawana haja ya kufuatilia yale yote yanafanywa. Lao ni kunyamanza kama watu wanasubiri jambo ambalo hawajui latoka wapi,” alisema Nyamweya.

Mbunge huyo aliomba wanakandarasi ambao hawajalipwa na serikali ya kaunti kuenda kortini na kushtaki serikali ili walipwe pesa zao.

“Wanakandarasi mlifanya kazi na serikali haijawalipa na msipoenda kortini, hamtaona pesa zenu. Nawaomba muende mshtaki serikali ya Kisii ili mlipwe,” aliongezea Nyamweya.