Share news tips with us here at Hivisasa

Baada ya kamati ya kuchunguza utumizi wa pesa katika serikali ya Kaunti ya Kisii kuundwa, baadhi ya wawakilishi wa upande wa upinzani wakiongozwa na George Bibao na Elkanah Nyandoro wasema kamati hiyo si halali.

Kulingana nao, wanakamati hao 13 waliochaguliwa kuchunguza utumizi wa pesa za serikali ya kaunti hiyo hawatafanya kazi yao kikamilifu kwani wengi wao wako katika idara na nyadhifa zile zinastahili kuchungwuzwa jinsi zinatumia pesa.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, nje ya makao ya bunge mjini Kisii, wawakilishi hao walisema kuwa baadhi ya wale ambao walichaguliwa kwa kamati hiyo walikuwa katika kamati ile ya kwanza ambayo ilivunjwa kufuatia utepetevu wa kikazi.

“Hawa ambao walichaguliwa kwa kamati ya kuchunguza utumizi wa pesa za serikali wao wenyewe wanastahili kuchunguzwa. Itakuwa aje ili wajichungeze wao wenyewe? Hilo haliwezekani na sisi tumeona huenda uwazi usionekane kamwe katika serikali yetu ya Kaunti ya Kisii,” alisema Bibao, mwakilishi wa wadi ya Bokimonge.

Wawakailishi hao wamemtaka mwenyekiti wa kamati hiyo ya kuchunguza utumizi huo Ronald Onduso kuwasilisha ripoti ya 'auditor general' ya mwaka 2013 hadi 2014 kwa bunge la kaunti hiyo chini ya wiki mbili zijazo ili kujadiliwa bungeni