Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamke mmoja ameshtakiwa katika mahakama moja mjini Eldoret kwa kosa la kuuza pombe haramu.

Elizabeth Chekomokwo alifikishwa katika mahakama hiyo siku ya Ijumaa kwa kosa la kuuza zaidi ya lita 50 ya kangara na lita tano ya chang’aa katika eneo la Kesses katika Kaunti ya Uasin Gishu.

Mahakama ilielezwa kuwa mshtakiwa alikuwa muuzaji sugu aliyekuwa akitafutwa na askari.

Mshtakiwa huyo alijitetea mbele ya Hakimu Mkuu Mkaazi Pauline Mbulika kwa kusema kuwa yeye ndiye tegemeo katika familia yake.

Mahakama iliamuru alipe faini ya Sh35,000 ama atumikie kifungo cha miezi sita gerezani.

Kwengineko, mwanamume mmoja alishtakiwa katika mahakama hiyo baada ya kupatika na zaidi ya lita 100 ya chang'aa.

Mahakama ilielezwa kuwa mshtakiwa amekuwa akitekeleza biashara hiyo haramu katika eneo la Chepketiny katika kaunti hiyo na amekuwa akisakwa na polisi.

Mshtakiwa aliamuriwa kulipa faini ya Sh60,000 au atumikie kifungo cha mwaka mmoja gerezani.