Waziri wa afya katika kaunti ya Kisii Sarah Omache amewaomba wakazi wote kutolipia ambulensi wakati gari hizo zinapowasafirisha wagonjwa hadi hospitali ya rufaa na mafunzo iliyoko mjini Kisii.
Hii ni baada ya wakaazi kulalamika kuwa wanalipia nauri gari hizo za ambulensi, madai ambayo waziri huyo alikanusha, huku akiwasihi wale wanao malalamishi sawia na hayo apige ripoti kwa afisi husika, akisisitiza kuwa huduma ya usafiri hupeanwa bila malipo.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano nje ya ofisi yake iliyoko katka hospitali hiyo, Omache alisema huduma ya usafiri hutolewa bila malipo.
“Naomba mkaazi yeyote wa kaunti ya kisii wakati anahitishwa pesa haswa na wahudumu wa gari la ambulensi ambalo husafirisha wagonjwa kutoka mahali popote pale, haswa katika kaunti ya kisii asilipe hata shilling, akiiitishwa apige ripoti kwangu,” alisema Omache.
“Serikali ya kaunti ndio hugharamia nauli, bali si mkaazi jinsi wengine walisema hapo awali, hayo ni mambo yasiyo ya ukweli,” aliongezea.
Hatua hii itawasaidia wakaazi wa kaunti hiyo, ambao wamekua wakilalama kwa kutakikana kulipa nauli ili kusafirisha wagonjwa.