Baadhi ya watu walioathirika na funza katika wadi ya Bomariba Kaunti ya Kisii walihudumiwa na shirika la msalaba mwekundu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na shirika hilo watu wengi wameathirika na funza katika maeneo ya Kaunti ya Kisii na ile ya Nyamira. 

Akiongea hiyo jana mhudumu  wa afya ya jamii katika sehemu hiyo Kepha King’oina watu wengi hasa wazazi hupuuza mafunzo maalum ya jinsi ya kujingika na funza.

Kulingana na King'oina wengi wa wale waliojitokeza katika shughuli hiyo walikuwa watoto.

Mhudumu huyo aliwaomba wazazi kutokea wakati kuna shughuli kama hiyo iliwaweze kusaidika.

“Tunaomba kuwa wakati watoto wanapokuja katika shughuli ya huduma kama hii ni bora mzazi  kufika  ili kusaidia na kutuonyesha nyumbani yake ili tuweze  kunyunyuza dawa na kuwauwa wadudu hawa,”alisema King’oina.

Chifu wa lokesheni hiyo Omae Nyang’au alisema kuwa wazazi hao wanahitaji kupewa funzo maalum jinsi ya kukabiliana na funza hao.

Nyangau pia aliwaomba manaibu wa machifu na wazee wa vijiji kuwa mstari wa mbele kuwafahamisha wazazi hao nakutenga siku moja ili wahudumu hao wafike mahala hapo nakutoa funzo hilo.

“Nimewambia manaibu wangu na wazee wa vijiji kuweka wazazi wote pamoja ili wahudumiwe. Wanapaswa kupata funzo ya jinsi ya kukabiliana na janga hili la funza,”alisema Omae.