Wanaume wembamba wamewekwa kando na wanawake wengi mara nyingi kwa sababu akina dada hawajui uzuru wao katika mahusiano.
Kikundi hiki cha wanaume kinaweza kufanya maisha ya mapenzi kwa mwanamke yawe riwaya yenye manto ya ajabu.
Sababu zifuatazo zitakufanya ufuate huyo mwanaume mwembamba ambaye haumpi jicho:
Anakufanya uhisi uko mkubwa na ujiamini
Kwa wewe mwanamke mwenye mwili mdogo, wembamba wa mumeo waweza kusadia usitafakari sana kuhusu kimo chako. Aidha, mwamume huyu atakusaidia udhibiti uzito wako kwa sababu ukianza kunenepa kupita kiasi ataanza kuonekana mdogo kama siafu kwako.
Atakula chakula chako kwa wingi
Kati ya furaha kuu za mwanamke ni kuona mumewe akila chakula alichoandaa. Baadhi ya wanaume wa aina hii wanapenda kula sana.
Ucheshi na utani
Wengi wa wanaume ambao ni wembamba ni wacheshi na pia waweza watania. Uko huru kukejeli maumbile yao lakini lazima upime kiwango chake cha hasira. Ikiwa ni mwepesi wa hasira, usimjaribu kwa kumueleza jinsi alivyokondo.
Utamsaidia kitandani na mukifanya ununuzi
Ni hakika kwamba wanaume wanapenda kuwa madereva kitandani lakini kusaidiwa ni ishara ya mapenzi. Hata kama unamuhurumia kwamba kazi hii utamvunja, watu huonea huruma wale wawapendao.
Vile vile, wakati mnafanya ununuzi wa nyumbani waweza msaidia kubeba bidhaa mlizonunua. Hii ni picha ambayo itatamanika na wapenzi wengi.