Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho amezungumzia uhusiano wake na Rais Uhuru Kenyatta miezi kadhaa baada ya wawili hao kutupilia mbali chuki yao ya kisiasa.
Wawili hao walikuwa adui wakubwa wa kisiasa, jambo lililosababisha Kenyatta kumuonya vikali naibu mkuu huyo wa chama cha ODM, kwamba atamyoosha vilivyo.
Joho alikua na mazoea ya kumkashifu Kenyatta pamoja na serikali yake kwamba imewafanya wapwani kutengwa huku ikiwafyonza wakenya pesa kupitia njia za ufisadi.
Hata hivyo, wawili hao walipatana wakati wa kuifungua barabara ya Dongo Kundu kule Bonje, Mariakani mwezi Juni mwaka huu na kuahidi kushirikiana.
Soma: Joho present as Uhuru launches iconic Dongo Kundu bypass
Akizungumza Jumanne wakati wa ufunguzi wa hafla ya Pili ya Uhamasishaji wa Ugatuzi (Second Devolution Sensitization Week) katika uwanja wa Makadara, Joho alisema yeye na Kenyatta huzungumza mara kwa mara.
Soma: Why Joho is demanding whooping Sh9 bln from Jubilee gov't
Aliongezea kuwa wawili hao wako karibu zaidi kuliko wavyokuwa hapo awali, kutokana na uhusiano mzuri wake aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa upinzani Raila Odinga na Rais Kenyatta.
"Makutano (handshake) yake Kenyatta na Odinga yamebadili na yatazidi kubadili mambo. Siku hizi nazungumza vyema na Rais Kenyatta. Kitambo hatukuwa twazungumza," alisema Joho.
#hivisasaoriginal