Mnamo Jumapili, rais Uhuru Kenyatta alishuhudia kutiwa saini kwa mkataba wa makubaliano kuhusu maswala ya uongozi na usalama yanayokusudiwa kurejesha amani katika taifa jirani la Sudan Kusini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kenya imekuwa mshirika muhimu miongoni mwa nchi wanachama wa IGAD katika utaratibu wa kurejesha amani na uthabiti katika taifa hilo changa la barani Afrika kwa imani kwamba amani na uthabiti nchini humo vinachangia ufanisi wa eneo hili lote.

Sherehe hiyo ilishuhudiwa na marais Yoweri Museveni (Uganda), Ismael Omar Guelleh (Djobouti), rais msimamizi Omar al-Bashir (Sudan) na Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khayre. Rwanda iliongozwa na Waziri wa nje Louise Mushikiwabo.

Kulingana na mkuu wa mawasiliano kwenye Ikulu, Kanze Dena, Rais Kenyatta kwa mwaliko wa Rais DonaldTrump atatembelea nchi ya Marekani kwa ziara rasmi mnamo tarehe Agosti 26, mwaka huu.

"Mkutano wa viongozi hao wawili unalenga kukuza uhusiano bora kati ya Kenya 🇰🇪 na Marekani 🇺🇸, hasa katika kuimarisha ushirikiano katika nyanja muhimu kama vile usalama, biashara na uekezaji na ushirikiano baina ya watu wa nchi hizi mbili," alisema Dena, alipowahotubia wanahabari kutoka Ikulu ndogo ya Mombasa, Jumatatu.

#hivisasaoriginal