Urembo umeleta mambo mengi mapya ikiwemo kutoboa sehemu za siri. Ikiwa una mpango wa kutoboa sehemu zako za siri, kuna mambo unastahili kujua. Aina hii ya urembo inaenziwa sana na wanawake lakini kuna asilimia ndogo ya wanaume ambao pia wanatoboa uume wao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kuna aina mbili za utoboaji kwa wanaume; ‘Jacob’s Ladder’ na ‘Prince Albert’. Ya kwanza inafanywa kwa kutoboa shimo mojo au zaidi katika sehemu ya chini ya uume wa mtu. Ile ya pili inatoboa karibu na kichwa cha pili cha mwanamume. 

Kwa upande wao, wanawake hupenda kutoboa kisimi.

Haya ndiyo madhara ya utoboaji wa kinembe au uume:

Inabadili ngono

Kutoboa kwa sehemu zako za siri kutabadili namna unafanya ngono. Kwa wanawake, itakulazimu uanze kupenda mwendo wa kobe au kadri ili usipate majeraha huko chini.

 Huu huwa mtihani mgumu kwa wale wanaoenzi kasi kama duma. Wanaume pia wanalazimika kuiga mbinu mbadala za ‘kutembea mbinguni’. 'Mpini' ambao umetobolewa hautafanya kazi kama kawaida.

Mambo haya yanafanya uamuzi wa urembo aina hii uwe na mambo mengi sana ya kuangaliwa vyema kabla ya kumtembelea msanii wa kubadili sehemu hizi.

Jeraha huchukua wiki 6-8 kupona

Unashauriwa kujua kwamba jereha linatokana na mageuzi haya huchukua wiki sita hadi nane kupona. Wakati huu utakuwa na ugumu kufanya mambo mengi ikiwemo kuenda haja ndogo. Kwa wanaume, ‘Prince Albert’ ni mbinu ambayo itakusumbua wakati huu wa kupona.

Ongezeko la kupata magonjwa ya zinaa

Uwezekano wa kupata magonjwa ya zinaa unaongeze ikiwa utakumbatia urembo huu. Hili linaadhiri sana wanaume kwa sababu kutumia kondomu itakuwa kizungumkuti haswa kama umeweka pete kwenye uume.

#MyLifestyle