Ubikira ni jambo zuri la kutamanika haswa katika mila na desturi za jamii za kiafrika. Watoto walishauriwa waweke zawadi hii hadi siku watakayofunga pingu za maisha.
Kwa bahati mbaya, wasichana pekee ndio wanalemewa wakati hali hii ya vijana inapoangaliwa wakati wa kupata jiko. Mila hii ina hatari zake zinazoletwa na ubikira na kukaa kwa muda bila ngono.
1. Saratani ya kibofu
Saratani hii itakua kimwili na pia kiakili. Matokeo ya utafiti yanaeleza kwamba wanaume wanaofanya ngono mara kwa mara wanapunguza uwezekano wa kupata saratani hii kwa asilimia ishirini (20%). Upungufu huu unatokana na ukweli kwamba 'kumwaga' mara kwa mara unatoa uchafu ulio kibofuni.
2. Mahusiano legevu
Wapo watu ambao wanaweza kuwa na uhusiano wa kufana bila ngono. Kwa upande mwingine, wachumba wengi hukosa furaha wakati ngono inakosekana ndoani. Jambo hili linaletwa na upungufu wa homoni inayowaweka wapenzi pamoja. Homoni hii hutolewa na mwili watu wakijamiana. Wapo wanaoogopa kwamba wenzao watatafuta pahala pengine pa kupunguzia uchu wa ngono.
3. Ongezeko la wasiwasi
Watu ambao hawana fursa ya kufanya ngono mara kwa mara husongwa na mawazo mengi kwa sababu ya wasiwasi usiyokuwa na msingi. Hili tatizo linatokana na kutokuwa na homoni za ‘endorphins' na 'oxytocin’ ambazo husaidia mtu kufurahi. Hizi homoni zinatolewa na mwili wako ukijamiana.
4. Kushikwa na mafua na homa
Ngono ni aina ya matibabu. Kitendo hiki kinasaidia mfumo wa kinga mwilini mwako kupigana na magonjwa yakiwemo mafua na homa. Ikiwa utafanya ngono mara mbili ama moja kwa wiki, virusi vitapigwa vitu kwa urahisi kutumia ‘immunoglobulin A’ inayoongezwa wakati wa aha hii.
Kwa kumalizia, hakikisha umejikinga kila wakati unapofanya ngono na uwe mwaminifu kwa mpenzio. Jilinde ili ulinde uwapendao na wanaokupenda.
#MyLifestyle