Wapo wanawake ambao huamua kuwa washiriki wa siri katika mahusiano ya wawili wapendanao. Kuna wale ambao wanaenzi mchezo huu. Zifuatazo ni sababu nne ambazo zinawafanya kina dada wawalazimishe waume wawachukue kama bibi wa tatu kuendelea.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kuogopa upweke

Wanadamu wanapenda kuishi katika jamii. Upweke unaogofya watu wengi haswa wanawake. Wasichana wanaweza kuamua kujamiana na mume yeyote wakati wowote wanapohisi upweke. Hawatataka kujua ikiwa mume huyu ameo au la. Uoga huu umeongeza idadi ya wasichana wanaovunja ndoa za wenzao.

Msukumo wa kifamilia

Msukumo kutoka kwa familia unawafanya baadhi ya wanawake 'waokote wanaume barabarani' na kuwapeleka nyumbani. Wao huamua kufanya hivi ili kutuliza maswali ya lini wataolewa. Katika harakati ya kutafuta yule ambaye watapeleka nyumbani, hawachagui kwa misingi ya mume kuoleka au ukapera.

Kutojithamini

Kuna kikundi cha wasichana ambao hawajithamini. Kikundi hiki kinaamini kwamba nafasi ya ‘mpango wa kando’ ni yao. Kati ya vyanzo vya imani hii ni wakati mume wanaomtaka anawaambia kuwa hawawezi kuwa mabibi wakutambuliwa na jamii yake.

Kujionyesha

Kuna wivu ambao wasichana fani wanao wakiwaona wenzao kwenye uhusiano mwema. Hisia hii inawalazimu kuanza kuonyesha mahusiano ya kimapenzi hata kama hayapo ili wasionekane wameachwa nyuma. 

Wanawake kama hao watachukua mume yeyote hata kama ameoa na kuonyesha wenzao kuwa wanachumbiwa. Wao hawajali litakalotokea ikiwa bibi wa mume waliyeiba atagundua shughuli hii ya kando.

#MyLifestyle